Home Simba SC HUYU MORRISON SIO POA KABISA….

HUYU MORRISON SIO POA KABISA….


IMEELEZWA kwamba winga wa Simba, Bernard Morrison ni masta wa kuusoma mchezo akianzia benchi badala ya kuanzishwa kipindi cha kwanza kinachokuwa kigumu kwake kuisaidia timu kupata matokeo.

Aliyekuwa beki wa timu hiyo, Kasongo Athuman alimfananisha Morrison na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Michael Paul kwamba alikuwa hatari akicheza dakika 45 baada ya hapo alikuwa anatembea tu uwanjani na mara nyingi alikuwa akiomba mabadiliko.

“Morrison ni masta wakusoma mchezo kama Paul ambaye akiingia kipindi cha pili alikuwa hatari na waliomuona wanalijua hilo, ndicho ninachokiona kwa mchezaji huyo wa sasa.

“Ni kitu kizuri kwa wachezaji wengine kutambua umuhimu wao wa uwepo benchi kwamba wakati mwingine wao ndio wanakuwa wameshika matokeo ya timu, hilo linaonyesha Morrison muda wote anakuwa mchezoni,” alisema.

Naye beki wa zamani wa timu hiyo, Frank Kasanga ‘Bwalya’ ni kama alipigilia msumari kauli ya Athuman kwamba Morrison ni mzuri anayetambua dakika 90 za mchezo zina maana gani kwake.

Alisema kwa upande wake anamuona Morrison aanze ama aanzie benchi anakuwa na jipya ndani ya uwanja kila wakati na kwamba ana uwezo wa kuzunguka uwanja mzima kusaka mipira na kutafuta nafasi ya kufunga.

“Morrison ni kati ya wachezaji wanaowapa mashabiki matumaini akiwemo uwanjani. Anajua kufunga mabao mazuri, kutoa pasi za mabao, kifupi anakosha mioyo na ana akili ya haraka ya kuwasoma wapinzani na kujua afanye nini na kwa wakati gani,” alisema Kasanga.

Hadi sasa amehusika kwenye mabao nane kwenye Ligi Kuu, akifunga mabao manne na kutoa asisti nne.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWASUMBUA ZAMBIA...MABOSI SIMBA WAULIZIA MKATABA WA WINGA 'KISHADA'...