Home Simba SC MEDDIE KAGERE BADO NI MNYAMA, KAHATA KURUDI SIMBA

MEDDIE KAGERE BADO NI MNYAMA, KAHATA KURUDI SIMBA


 WAKATI mshikaji wake ambaye walicheza naye pamoja ndani ya kikosi cha Gor Mahia ya Kenya, Francis Kahata akiwaaga mashabiki wa Simba baada ya dili lake kuisha, habari zinaeleza kuwa Meddie Kagere ameongeza dili kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Meneja wa Kagere, Patrick Gakumba hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa mkataba wa Kagere mwenye mabao 11 ndani ya ligi msimu huu wa 2020/21 unakaribia kuisha msimu utakapomeguka jambo ambalo lilileta mvurugano.

Kutokana na ishu hiyo, Kagere alikuwa anahusishwa kwenda Yanga pamoja na Azam FC ili akaendelee maisha yake ya soka ndani ya ardhi ya Bongo.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Simba zimeeleza kuwa Kagere bado yupo Simba ila Kahata hatakuwepo msimu ujao kwa kuwa mkataba wake umeisha na hajaongezewa dili lakini kuna uwezekano akarudi Simba wakati ujao.

“Ukweli ni kwamba wengi wanatuvuruga kwa sasa kuhusu Kagere, mkataba wake ni mrefu na atabaki kuwa mali ya Simba mpaka pale tutakapoamua kumuuza.

“Ikiwa watani zetu wanahitaji saini yake bado hatujapata taarifa zake ila ukweli ni kwamba bado yupo ndani ya Simba mpaka 2024, kuhusu Kahata yeye hajaongezewa mkataba lakini anaweza kurudi wakati mwingine” ilieleza taarifa hiyo.

Kagere amekuwa na ushkaji mkubwa na benchi msimu huu wa 2020/21 ambapo nafasi yake amekuwa akianza mshikaji wake Chris Mugalu na wakati mwingine nahodha wake John Bocco.

Kuhusu suala la kuanza kikosi cha kwanza, Kocha Mku wa Simba, Didier Gomes alisema kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi hicho ni muhimu na anafaa kuanza kikosi cha kwanza.

Ni Kahata mwenyewe ambaye ni mchezaji wa kwanza kuagwa na Simba baada ya mkataba wake kuisha ambapo waliweka wazi kwamba anaweza kurudi wakati mwingine. 

SOMA NA HII  MAGOLI BORA CAF: FRIII KIKI YA CHAMA YAPIGIWA SALUTI CAF...ULE MSHUTI WA KANOUTE SASA