Tetesi za usajili

HUYU HAPA KIUNGO MKABAJI WA KAIZER CHIEFS ANAYEPIGIWA HESABU NA YANGA

admin June 13, 2021 5:47 am


 IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumsajili kiungo mkabaji anayecheza ndani ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.

Nyota ambaye anapigiwa hesabu na Yanga anaitwa Anthony Akumu, ambaye ameletwa duniani Oktoba 20,1992 ana umri wa miaka 28 ni mzaliwa wa Rachuonyo, Kenya.

Ikiwa dili lake litakamilika kwa sasa ambapo mpanga mipango ni Injinia, Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ndani ya Yanga kutia timu Afrika Kusini.

Kiungo huyo miongoni mwa timu ambazo amecheza ni pamoja na Gor Mahia mwaka 2010-14, 2014-15, alikuwa ndani ya Al Khartoum, 2016-20 aliitumikia Zesco United na sasa yupo Kaizer Chiefs.

Pia katika timu yake ya taifa ya Kenya, kiungo huyo amecheza jumla ya mechi 38.

INJINIA YUPO KAZINI, UJANJA WA KAGERE WAANIKWA, NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI CHIKWENDE PERFECT AWAGAWA SIMBA ISHU YA KUVUNJIWA MKATABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply