news

OSCAR OSCAR, KARIA, KIMJI AMBAO NI WAGOMBEA TFF, KESHO MAJINA KUWEKWA HADHARANI

admin June 15, 2021 2:47 pm


KESHO Juni 16 inatarajiwa kuwekwa wazi juu ya wagombea ambao wamepenya hatua ya uchaguzi katika Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Mchakato wa uchaguzi kwa sasa unaendelea ambapo Juni 12 ilikuwa ni mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kwa wagombea.

Jumla ya wagombea 6 walikamilisha zoezi hilo kwa upande wa nafasi ya Urais ikiwa ni pamoja na Oscar Oscar, Wallace Karia ambaye anatetea kiti chake, aLLY Mayay, Ally Saleh, Evans Mgeusa na Hawa Mniga.

Pia ni wajumbe 26 ambao wanawania nafasi hiyo katika kanda 6 tofauti ikiwa ni pamoja na Jimmy Mshindo, Saady Khimji, Lameck Nyambaya, Liston Katabazi, Hosseah Lugano, Elisony Mweladzi na Athuman Kambi kwa kanda namba 1 ya Dar na Pwani.

Wengine ni Khalid Mohamed, Zakayo Mjema na Thabity Kandoro kwa kanda ya Arusha ambayo ni namba mbili.


Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa leo ni siku ya mwisho kwa kamati kukaa chini kupitia mchujo wa awali na kesho majina yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo. 

RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA WIKI HII VIDEO: RAIS AAGIZA WASANII KUANZA KULIPWA, VAT YA NYASI BANDIA YAONDOLEWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply