Home news ABDI BANDA ‘AMTOROSHA’ MKUDE NDANI YA SIMBA SC

ABDI BANDA ‘AMTOROSHA’ MKUDE NDANI YA SIMBA SC


UWEZO wa kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude ambaye hivi karibuni ameingia kwenye mvutano na klabu yake umemfanya beki wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akicheza Highland Park ya Afrika Kusini, Abdi Banda kumjadili kisha kumpa mchongo akimwambia anaweza kukiwasha Sauzi freshi!

Banda alisema anaamini kwa uwezo wa Mkude anaweza kuwa dili Afrika Kusini kama atakuwa na utayari kipindi kama hiki cha mwishoni mwa msimu kwenda kupambania nafasi.

“Huwa naona kuna wachezaji wengi tena sana nyumbani Tanzania kuwa wana uwezo wa kucheza Ligi ya Afrika Kusini (PSL),” alisema Banda aliyewahi kucheza na Mkude Simba kabla ya kwenda Afrika Kusini kukipiga Baroka na baadaye kuangukia Highland.

“Kipindi kama hiki kwa Sauzi wachezaji kutoka mataifa mbalimbali wanaenda kupambania nafasi za kusajiliwa, unaweza kuwa mchezaji mzuri lakini wao wakataka kukuona kama ni kweli au laa, niliwahi siku moja kuwa napigania namba sehemu ya kusajiliwa na mchezaji ambaye ametoka kufanya majaribio Marseille,” alisema beki huyo kiraka na kuongeza na kuongeza;

“Tulipambana na tukabaki wawili, mimi na yeye na walikuwa wakitaka beki mmoja wa kati, jamaa aliondoka maana kuna dili lake jingine lilijipa la hela nyingi, kwa uwezo wa Mkude anaweza kufanya makubwa Sauzi kama ataamua.”

SOMA NA HII  KWA REKODI HIZI SIMBA WASHINDWE WENYEWE TU