Habari za Yanga
Habari za michezo

ZA NDAANI KABISAAA…YANGA WALIIZIDI SIMBA HAPA KWA JOB….LA SIVYO ANGEKUWA MSIMBAZI …

admin September 7, 2023 10:06 am

Mchambuzi Clouds FM, Frahan Kihamu amesema kuwa Klabu ya Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili beki, Dickson Job wakati akiwa Mtibwa Sugar lakini walizidiwa ujanja na wapinzani wao Yanga SC.

Job alisajiliwa Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili msimu wa mwaka 2020/21 akitokea Mtibwa ya Morogoro baada ya kuonyesha kiwango bora na Serengeti Boys kisha akasajiliwa na Walima Miwa hao akitokea Moro Kids.

“Dickson Job, Mchezaji ambaye Simba walikuwa wa kwanza kutambua ubora wake na ndio timu ya kwanza kuwasiliana na Mtibwa ili akakipige makutano ya Uhuru na Msimbazi.

“Ni makosa kidogo tu ya kiufundi yalitokea na Kijana akaenda Yanga, kazi nzuri na nzito sana ya Mwenyekiti aliyepita Dr Mshindo Msolla aliyeenda front sana na deal likatimia akaenda Jangwani.

“Moja kati ya Wachezaji ambao siku akistaafu nitaandika visa vyao tukijaaliwa uhai, one of the best,” amesema Frahan Kihamu.

MCHAMBUZI:- TUSIJIDANGANYE…TAIFA STARS NI WAKAIDA MNOO MBELE YA ALGERIA…. KAMA ULIKUWA HUJUI….’MWAMBA’ HUYU YUKO NYUMA YA DILI LA NOVATUS KUTUA SHAKTAR…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply