Simba SC

KIUNGO SIMBA ANUSURIKA KUACHWA, GOMES AMBAKISHA

admin June 18, 2021 9:47 pm


 MUDA na wakati wowote Simba itamuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake mshambuliaji Miraji Athumani ‘Sheva’ wa kuendelea kukipiga Msimbazi.

 

Awali kiungo huyo alikuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaochwa katika kuelekea usajili wa msimu ujao ambao wanajiandaa na michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.

 


 Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, kimeliambia Championi Jumatano kuwa, Sheva amebakishwa kuendelea kukipiga katika timu hiyo baada ya kocha Mfaransa Didier Gomes kupendekeza abaki.

 

Kilisema kuwa kiungo huyo amebakishwa baada ya kocha kushawishika na kiwango chake akiamini kitaongezeka hapo baadaye baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha aliyoyapata.

 

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kikubwa kocha hataki kuwaacha rundo la wachezaji wengi, hivyo atawabakisha wale ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri.

 

“Sheva ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha atawaacha katika usajili wa msimu ujao, ni baada ya benchi la ufundi kupendekeza kumbakisha Simba.

 

“Na anaachwa baada ya tathimini kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi wakiamini bado Sheva yupo vizuri, lakini kiwango kilishuka hapa katikati baada ya kupata majeraha ambayo hivi sasa amepona.

 

“Sheva ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu pamoja na akina Ibrahim Ajibu na Gadiel Michael ambao hao tayari wameachwa,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Simba kwa kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ hivi karibuni alifanya mazungumzo na gazeti akizungumzia usajili alisema kuwa: “Masuala yote yanayohusu usajili tumewaachia benchi la ufundi.


“Na ripoti ya usajili bado haijakabidhiwa kwa uongozi mara baada ya kuipata tutaanza kuifanyia kazi sehemu ya utawala.”


MCHEZAJI CONGO AIPIGA CHINI TP MAZEMBE KISA OFA YA YANGA BAADA YA KUMKOSA MANYAMA, SIMBA YAMGEUKIA BEKI HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply