Yanga SC

BEKI MCONGO ALIYEJIFUNGA YANGA MIAKA MIWILI ATAJA NAMBA YA JEZI ATAKAYOVAA

admin June 20, 2021 3:47 am


NYOTA wa AS Vita, Djuma Shaban amesema kuwa akijiunga na Klabu ya Yanga baada ya uataratibu wa dili lake kukamilika atahitaji kuvaa jezi namba 21.


Beki huyo raia wa Congo inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Yanga kwa dili la miaka miwili ambapo amesema kuwa akija anahitaji kuvaa jezi namba 21.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa dili lake na AS Vita linameguka Juni 30 hivyo ikiwa atakuja Bongo basi atafanya kazi na mabosi wake wapya kwa ajili ya kuyatafuta mafanikio.

Kwa upande wa wachezaji wa Simba ameweka wazi kwamba hakuna ambaye anamvutia kwa sasa licha ya kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
KIUNGO MZIMBABWE MIKONONI MWA SIMBA, INJINIA AIBUKIA MALI SIMBA YABAKIZA DAKIKA 180, MZEE WA KUKERA MORRISON AKASIRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply