kimataifa

BARCELONA YAMALIZANA NA MAJEMBE MANNE

admin June 21, 2021 7:47 am


 TIMU ya Barcelona imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha dili la miaka miwili kwa mshambuliaji Memphis Depay kutoka Lyon.

Timu hiyo ilikuwa inaipigia hesabu saini ya nyota huyo kwa muda mrefu na mwisho wa siku walifanikiwa kumpata mchezaji huyo na kumpa dili la miaka miwili ataondoka hapo mwaka 2023 ikiwa mabosi hao hawatakuwa tayari kumpa dili jipya.

Staa huyo alijenga jina lake akiwa ndani ya Manchester United kabla hajatua Lyon hivi karibuni aligoma kusaini dili jipya na timu hiyo ya Ufaransa.

Anakuwa ni mchezaji wa nne Barcelona inayonolewa na Kocha Mkuu, Ronald Koeman kusajiliwa kwenye usajili huu baada ya kuanza na Sergio Arguero, Eric Garcia na Emerson Royal.  


KATUMBI NOMAA..ATIA MKONO USAJILI WA YANGA.. MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAREJEA KAZINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply