KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina, leo Juni 23 kinaanza safari kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali unatarajiwa kuchezwa Juni 26, Uwanja wa Majimaji, Songea.
Kikosi hicho kinaondoka na ndege, Uwanja wa Julius Nyerere. Ikumbukwe kwamba mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambao utawakutanisha Biashara United v Yanga.
Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini kwamba watapata ushindi.
Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambapo walitwaa msimu uliopita kwa kushinda mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa fainali.