Azam FC

NYOTA WAWILI WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA, SONGEA

admin June 24, 2021 9:47 am


 NYOTA wawili wa Azam FC watakosekana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba, Juni 26, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ila watawakosa wachezaji wawili ambao wanasumbuliwa na majeraha.

“Yahya Zaydi na Ally Niyonzima hawa wamebaki Dar kwa kuwa wanasumbuliwa na majeruhi hivyo hawatakuwa kwenye kikosi chetu dhidi ya Simba.

“Kuhusu maandalizi yetu tupo tayari na kila mmoja anahitaji kupata matokeo chanya hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi na kwa namna abavyo wametupokea wanastahili shukrani,” amesema.

Mshindi wa mchezo huo kati ya Simba v Azam FC atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United v Yanga utakaochezwa kesho, Juni 25. 

AZAM FC YARUDISHA SHUKRANI KWA MASHABIKI, MAPOKEZI YAO ACHA KABISA EDEN HAZARD HAELEWI KAMA ANAWEZA KUREJEA KWENYE UBORA WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply