Home kimataifa UEFA YAFUTA SHERIA YA BAO LA UGENINI

UEFA YAFUTA SHERIA YA BAO LA UGENINI


 SHIRIKISHO la Soka Ulaya (Uefa) limetangaza kufuta sheria ya bao la ugenini ambayo ilikuwa inatumika kwenye michuano ambayo inaandaliwa na Uefa sheria hiyo ilianza kutumika tangu mwaka 1965.

 

Sheria hiyo ilikuwa inatumika kuamua matokeo baada ya raundi mbili  nyumbani na ugenini, baada ya kufuta sheria hiyo na baada ya kuchezwa  raundi mbili, endapo   matokeo yakiwa sare, basi zitaongezwa dakika 30 na baadaye mikwaju ya penati.

 

Timu kadhaa ikiwemo Chelsea, Manchester City na PSG kwa nyakati tofauti walikuwa wahaga wa sheria hiyo  baada ya kujikuta wakitupwa nje ya michuano kutokana na timu pinzani kunufaika  kwa faida ya goli la ugenini.

 

Kwa mujibu wa Rais wa Uefa Aleksander Ceferin amesema goli la ugenini limefanya timu nyingi kucheza kwa kujilinda kwa sababu ya faida ya bao la ugenini.

SOMA NA HII  CHELSEA KUMSHUSHA MANE NA POCHETTINO STAMFORD BRIDGE...