YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar kwa sasa anawasubiri Yanga ili aweze kusaini dili jipya kwa ajili ya kuwatumikia kwa msimu ujao wa 2021/22.
Habari zimeeleza kuwa nyota huyo licha ya kuwa bado ana dili la mwaka mmoja ndani ya Kagera Sugar anafikiria kuondoka ikiwa atapata dil jipya.
“Mhilu bado yupo Kagera Sugar lakini anaweza kuondoka ikiwa atapata ofa kubwa na malengo yake ni kuweza kupata changamoto mpya hivyo kwa sasa anasubiri mabosi wa Yanga na Azam FC waweze kukamilisha mpango wao,” ilieleza taarifa hiyo.
Mhilu mwenyewe aliliambia Championi Jumatatu kwamba anahitaji kupata changamoto mpya iwe ndani ya Bongo ama nje yeye yupo tayari kucheza.
“Ninafikiria sana kwenda kucheza nje ya nchi ili kuwa imara zaidi ya hapa lakini imani yangu ni kwamba inawezekana na ninaweza. wa kuwa nina kipaji na uwezo mkubwa,” alisema Mhilu mwenye mabao.
Imekuwa ikieelezwa kuwa Mhilu ambaye aliwahi kucheza ndani ya Yanga yupo kwenye mpango wa kusajiliwa na mabosi wake hao wa zamani ambao kwa sasa wananolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.