Home Simba SC AME AKINGIWA KIFUA SIMBA

AME AKINGIWA KIFUA SIMBA

 


KUFUATIA kuwepo kwa taarifa kuwa beki wao Ibrahim Ame anaweza kutolewa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu, Uongozi wa klabu ya Simba umeibuka na kuweka wazi kuwa mchezaji huyo ataendelea kuichezea Simba na kama kuna taarifa tofauti zitatolewa na kocha mkuu wa kikosi hicho, Didier Gomes na si mtu mwingine.

Ame amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Simba mara kwa mara, kutokana na ushindani mkubwa wa namba katika nafasi anayocheza ya mlinzi wa kati.

Ukiachana na Ame Simba ina mabeki wengine wanne wa kati ambao ni; Kennedy Juma, Pascal Wawa, Joash Onyango na Erasto Nyoni ambaye mara kadhaa amekuwa pia akipewa majukumu ya kucheza kama kiungo mkabaji.

Akizungumzia ishu ya Ame, Mkuu wa maudhui wa klabu ya Simba, Ally Shatry amesema: “Ni kweli kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu baadhi ya nyota wetu kuhusishwa kutolewa kwa mkopo akiwemo beki wetu Ibrahim Ame.

“Lakini uhalisia wa jambo hilo ni kwamba, kwanza watu wanapaswa kufahamu kuwa Ame ni mchezaji wa Simba, na maamuzi yeyote juu ya wachezaji wa Simba hasa kuhusiana na suala la kucheza yapo kwa kocha mkuu Didier Gomes, yeye ndo anaweza kuzungumzia masuala hayo na si mtu mwingine kama siyo kwa ruhusa ya kocha.”

SOMA NA HII  MKATA UMEME WA SINGIDA BIG STAR 'AIWANGIA' SIMBA MECHI YAO YA KESHO...