Home EURO 2020 EURO 2020, UBELGIJI V URENO KITAWAKA LEO

EURO 2020, UBELGIJI V URENO KITAWAKA LEO


LEO Juni 27 ndani ya Euro 2020 unatarajiwa kuchezwa mchezo mkali kati ya Ubelgiji dhidi ya Ureno ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 4:00 usiku ikiwa ni wa hatua ya 16 bora.

Itakuwa ni Uwanja wa La Cartuja de Sevilla na rekodi zinaonyesha kwamba Ureno ya Cristiano Ronaldo ikiwa haijapoteza mbele ya Ublegji katika mechi tano zilizopita.

Pia rekodi zinaonyesha kwamba Ublelgiji yenye Romelu Lukaku inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Martinez katika mechi 58 ni mara mbili imekamilisha dk 90 bila kufunga bao lolote na ilikuwa ni mbele ya Ufaransa kwenye Kombe la Dunia na mbele ya Ureno Juni 2018.


Ureno ilikuwa kundi F ambapo ilishinda mchezo mmoja na ilipoteza mchezo mmoja sawa na sare moja huku Ubelgiji ambayo ilikuwa kundi B ilishinda mechi zote tatu ilifunga mabao 7 na kuruhusu bao moja.

SOMA NA HII  ROONEY AMPIGA BENCHI GREALISH, AANZA NA RASHFORD DHIDI YA UJERUMANI