Home Simba SC MKUDE AMUAGA KAHATA FRANCIS

MKUDE AMUAGA KAHATA FRANCIS


KIUNGO mkabaji wa Simba, Jomas Mkude amemuaga mshikaji wake Francis Kahata ambaye ameaga rasmi kwa mashabiki na viongozi wake kwa muda ambao alikuwa ndani ya kikosi.

Kahata amekuwa mchezaji wa kwanza kuaga Simba baada ya kandarasi yake ya miaka miwili kumeguka ndani ya kikosi hicho.

Jana nyota huyo aliwaaga mashabiki na wachezaji wenzake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kueleza kuwa anakwenda kuanza changamoto mpya.

Mkude amesema kuwa ni wakati mgumu ila lazima ufike kwa kuwa ni hatua ya maisha lakini atamkumbuka  Kahata.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA VIGOGO WA FIFA NA CAF KUTUA SIMBA KUMBE MCHEZO MZIMA UKO HIVI AISEE..