Home epl RAHEEM AIGOMEA CITY KUWA CHAMBO

RAHEEM AIGOMEA CITY KUWA CHAMBO

[the_ad id="25893"]


MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Raheem Sterling hana mpango wa kuondoka hapo ili timu hiyo iweze kupata saini ya mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

Imekuwa ikielezwa kuwa City ina mpango wa kupata saini ya Kane huku ikiwaweka chambo baadhi ya wachezaji wake na inatajwa kuwa Sterling ni mmoja wapo.

Mkwanja ambao City inayonolewa na Pep Guardiola wametenga mezani ni milioni 100 pauni ila zimekataliwa na bosi wa Tottenham, Daniel Levy ambaye anataka zaidi ya fedha hizo jambo ambalo limewafanya City kuwa na mpango wa kuwapa wachezaji wawili.

Taarifa zinasema kuwa Sterling amegomea kutolewa kwa mpango huo na ikiwa ataondoka ndani ya kikosi hicho itakuwa ni kwa mpango wake binafsi na sio wa timu kumtoa chambo ili wampate mchezaji.

SOMA NA HII  WAKATI AKIZINGUA MAN UTD....RONALDO AKAMILISHA UJENZI WA HOTEL LA KIFARAHI MOROCCO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here