Home Yanga SC YANGA WAZINDUA TAWI TABORA

YANGA WAZINDUA TAWI TABORA


 LEO Juni 23 Uongozi wa Yanga umezindua tawi jipya liitwalo Yanga Kwanza.

Taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga umeeleza kuwa:”Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko Eng. Hersi Said leo amezindua Tawi jipya liitwalo Yanga Kwanza.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mashabiki wa Yanga na wanachama wa tawi hilo lilipo Tabora pamoja na mashabiki.

Yanga ipo Tabora kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Biashara United ambao ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali utakaochezwa Ijumaa, Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi. 

SOMA NA HII  YANGA : BADO HATUJAKATA TAMAA, TUTAZIDI KUPAMBANA