Home Yanga SC YANGA YAMJUMUISHA KIPA WA KIKOSI B KWENYE MSAFARA

YANGA YAMJUMUISHA KIPA WA KIKOSI B KWENYE MSAFARA


KIPA Godfrey Magaigwa ambaye ni namba moja katika kikosi B amejumuishwa kwenye kikosi cha wakubwa kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Biashara United

Mchezo huo utapigwa Ijumaa, Juni 25, uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora

Yanga imeondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea Tabora kwa usafiri wa ndege na tayari imeshatia timu Tabora.

Magaigwa aliibuka kuwa mlinda lango bora wa ligi kuu ya Vijana iliyofikia tamati mwishoni mwa wiki iliiyopita

Vijana wa Yanga walitinga fainali ya michuano hiyo lakini wakapoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ni Mabingwa mara tatu mfululizo.


SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA SABABU YA NYOTA WAO WATATU KUUKOSA MCHEZO WA J/PILI..WAFUNGIWA NA CAF