OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Yanga, Julai 3 wanaweza kuwafunga mabao matatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ameweka wazi kuwa jambo la msingi kwa waamuzi ni kufuata kanuni na kwa namna walivyojipanga basi hazitapungua tatu.