Yanga SC

JEURI YA PESA: BAADA YA DILI LA DJUMA, YANGA WAPIGA SIMU AS VITA KUMTAKA MAKUSU

admin July 2, 2021 2:00 pm


YANGA sasa inazungumza na mshambuliaji wa AS Vita, Makusu Mundele ambaye nusu msimu uliopita aliichezea Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Mundele bado ni mchezaji halali wa Vita akiwa na mkataba wa mwaka mmoja Yanga. 

Soka la Bongo linafahamu kwamba ni ushauri wa Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wamewaambia mabosi wa Yanga na kocha wao Nesreddine Nabi kwamba hata kama jamaa hakufanya kitu Pirates asipuuzwe hapo Yanga atafanya mambo makubwa kama atakuja haraka.

Kisinda alicheza kwa mafanikio na Mundele wakiwa AS Vita na ushirikiano wao uliwahi kusababisha balaa zito kwa Simba ikikubali kipigo cha mabao 5-0 kabla hawajatenganishwa wakati Kisinda akitua Yanga huku Mundele akikwama dakika za mwisho kutua Morocco.

Tayari Tuisila kupitia Nabi amewaambia mabosi wake wamlete Mundele ingawa mabosi hao wanataka kutumia ukaribu wao na Vita kumchukua kwa mkopo. Kisinda alisema; 

“Nilikutana na Makusu (Mundele) akaniulizia juu ya kuja huku Tanzania, Ni mshambuliaji ambaye anajua kutafuta eneo zuri ili afunge mtu ambaye hapa kwetu (Yanga) tunamkosa. Siwezi kuogopa kumsajili Makusu kwa kuwa hakufanya vizuri Afrika Kusini hapa namuona atakuwa mtu muhimu atakayekubalika kwa haraka kutokana na timu tuliyonayo.”

VIDEO: MANULA, TUTAONYESHA UKUBWA WA TIMU UWANJANI ILI KUTWAA UBINGWA WAWILI WA SIMBA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply