Simba SC

WAWILI WA SIMBA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

admin July 2, 2021 2:47 pm

 NYOTA wawili wa Simba kesho wanatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. 

Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa kiujumla maandalizi yapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya kuwakosa wachezaji wawili.

“Ni Jonas Mkude ambaye matatizo yake yanajulikana pamoja na Ibrahim Ajibu ambaye anasumbuliwa na Malaria.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanahitaji ushindi, ” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 73 na Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67.

Mkude alisimamishwa na Simba kutokana na tatizo la kinidhamu ambapo anatakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya akili.


JEURI YA PESA: BAADA YA DILI LA DJUMA, YANGA WAPIGA SIMU AS VITA KUMTAKA MAKUSU YANGA:TIMU YETU NI BORA,TUTAPATA POINTI TATU ZA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply