Home Yanga SC NABI ATAMBA KUIKABILI SIMBA KWA KUTUMIA MBINU ZA KISUDANI

NABI ATAMBA KUIKABILI SIMBA KWA KUTUMIA MBINU ZA KISUDANI


KOCHA wa Yanga, Nabi Nasreddine amesema alikutana na Simba kwa mara ya kwanza msimu huu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo anafundisha El Marreikh ya Sudan.

Nabi alisema kuna baadhi ya vitu ambavyo alitumia katika mchezo ule uliochezwa Sudan na kumalizika kwa suluhu atavifanya tena katika mchezo wa Jumamosi na akasisitiza kwamba hazungumzi sana wao watatenda kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Kama ambavyo wao wanatamani kushinda, basi nasi ni hivyohivyo, tusubiri muda wa mechi ufike tuone namna gani ushindani ambao tutautoa na kupata kile ambacho tunahitaji,” alisema Nabi ambaye amekiri kusikia tambo za Simba kwamba watashinda mechi hiyo.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Tunisia na Ubelgiji, alipocheza mara ya kwanza na Simba iliyokuwa chini ya kocha Didier Gomes mechi licha ya kuisha kwa suluhu jijini Khartoum huko Sudan muda mfupi baadaye alifukuzwa kazi na ndio akatua kujiunga na Yanga.

Mechi ya kwanza ambayo alibidi akutane na Simba katika Ligi Kuu iliahirishwa Mei 8, kutokana na muda kusogezwa mbele licha ya kikosi chake kufika uwanjani kama ilivyokuwa imepangwa.

SOMA NA HII  AL MAREIKH TUMBO JOTO,GAMONDI AMVURUGA KOCHA