Azam FC

KIUNGO MZAMBIA AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

admin July 4, 2021 10:47 pm


RASMI mabosi wa Azam FC wamemalizana na kiungo wa Zambia Charlse Zulu kwa dili la miaka miwili.

Kiungo hiyo jana Julai 4 alifanyiwa vipimo na kuweza kufuzu hivyo wakafikia makubaliano ya kumpa kandarasi ya miaka miwili.

Alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini hivyo msimu ujao wa 2021/22 atakuwa ndani ya viunga vya Azam Complex.

Azam FC wamemalizana naye baada ya kufikia makubaliano na timu yake ya Cape Town City aliyokuwa akitumikia ambapo pia aliwahi kukipiga ndani ya Zanaco ya Zambia.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU YANGA: TUTAWAFUNGA TENA SIMBA KIGOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply