news

MTIBWA SUGAR:TUTACHEZA KAMA FAINALI MECHI ZETU

admin July 5, 2021 8:47 am


 KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Baraka Majogoro amesema kuwa watapambana katika mechi zao zilizobaki ili kupata matokeo chanya yatakayowafanya wabaki ndani ya ligi hivyo watacheza kama fainali.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 38 ipo nafasi ya 11 haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi kutokana na pointi walizonazo kuweza kufikiwa na Coastal Union iliyo nafasi ya 17 na pointi zake 34.

Akizungumza na Soka la bongo, Majogoro amesema kuwa wanatambua nafasi ambayo wapo nayo ni ngumu kuweza kubaki ikiwa hawatashinda hivyo wanachotakiwa ni kupambana.



“Ligi ni ngumu kwa sasa na kwa nafasi ambayo tupo hakuna ambaye anaweza kusema tupo salama. Kikubwa kilichobaki ni kuona kwamba mechi zilizobaki zote tunapambana kama fainali ili kushinda na kila kitu kinawezekana,” amesema Majogoro.

Mechi mbili za Mtibwa Sugar ambazo zimebaki ni Julai 14 dhidi ya Dodoma Jiji yenye pointi 42 na JKT Tanzania yenye pointi 36, Julai 18, zote zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

MZEE MPILI: TULIPASWA KUCHUKUA UBINGWA, SASA MPIRA KIGOMA KUMBE! KARIAKOO DABI TATIZO LILIANZIA KWENYE KUITWA WAKUOKOTWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply