Home news MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI SITA MAZIMA

MTIBWA SUGAR YAZITAKA POINTI SITA MAZIMA

 


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi mipango yao ni  kuhakikisha wanasalia katika ligi kuu kwa kubeba pointi zote sita za mechi zao mbili zilizobakia.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema kwamba wanatambua wapo kwenye nafasi ngumu ila watapambana kupata matokeo chanya.

โ€œTutaanza na Dodoma Jiji katika kuhakikisha tunachukua pointi zote sita zilizosalia katika ligi kuu ili tuepuke mstari wa hatari ambao unaweza kutukuta.

โ€œKikosi chote kipo tayari kwa mchezo huo, mashabiki waje waone soka la kuvutia na ukizingatia wakati huu timu zinatafuta alama kwa hali yote.โ€

Kwenye msimamo, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 imekusanya pointi 38 baada ya kucheza mechi 32.

SOMA NA HII  CHEZA PROMO YA NON STOP DROP KUPATA TSH MIL 450/=|SHIRIKI KWA KUCHEZA KASINO...