Home Yanga SC ORODHA YA NYOTA WANNE WA KIMATAIFA WANAOWINDWA NA YANGA HII HAPA

ORODHA YA NYOTA WANNE WA KIMATAIFA WANAOWINDWA NA YANGA HII HAPA


 IMEELEZWA kuwa Yanga itafanya usajili funga kazi kwa ajili ya kuhakikisha msimu ujao wanarudisha ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara kutoka kwa Simba, na wanafanya vizuri pia kimataifa.

 

Yanga mpaka sasa imeshakamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa kulia wa AS Vita, Djuma Shabani ambaye amesaini mkataba wa miaka 2.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Arafat Haji, alisema Yanga msimu huu lazima itafanya usajili wa wachezaji wasiopungua watano wa kimataifa ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inaenda kufanya vyema katika michuano ya kimataifa.


Jeuri hiyo ya Yanga ya kushusha vifaa vya maana inatokana na jeuri ya mkataba mpya waliongia hivi karibuni na Azam wenye thamani ya bilioni 34.8 ambao unawafanya kuwa fedha ya kutosha kwa ajili ya kusajili wachezaji bora barani Afrika.

 

Pia chanzo chetu cha kuaminika kutoka Yanga kimelipenyezea mchongo Championi Ijumaa kuwa baadhi ya wachezaji ambao wapo katika mipango ya kusajiliwa na Yanga ni Heriter Makambo (Horoya), Fiston Mayele (AS Vita), Henock Inonga (Motema Pembe) na kipa Eliezer Tape Iri.


“Yanga itafanya usajili wa wachezaji wa maana kwa ajili ya kufanya vyema katika michuano ya kimataifa na ndio maana utaona tayari tumeshakamilisha usajili wa beki wa kulia Shabani Djuma ambaye ana uzoefu mkubwa na michuano ya kimataifa.

 

“Hivyo baada ya yeye watakuja wachezaji wengine wazuri wa kimataifa, tayari tupo katika mazungumzo na wachezaji japo dirisha halijafunguliwa bado lakini sheria zinaturuhusu kufanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.

 

Wachezaji wanaotajwa kusajiliwa na Yanga mara baada ya Shabani Djuma ni beki wa kati wa DC Motema Pembe, Henock Inonga Baka, Heritier Makambo (Horoya), Fiston Mayele(AS Vita) na Kipa Eliezer Tape Iri (San Pedro FC).

 

Kama nyota hao watatua, hii itafanya Yanga itengeneze first eleven ya hatari kinoma, kutokana na rekodi za nyota hao.


Picha la first eleven linalovutwa na Yanga ni hili; kipa Eliezer, Djuma (beki kulia), Dickson Job (beki wa kati namba 4), Henock Inonga (Beki wa kati namba 5), Mukuko Tonombe (kiungo mkabaji namba 6), Tuisila Kisinda (winga kulia namba 7), Feisal Salum (kiungo mshambuliaji namba 8), Heriter Makambo (mshambuliaji wa kati namba 9), Fiston Mayele (mshambuliaji wa pili namba 10), Yacouba Songne (winga kushoto namba 11).

SOMA NA HII  MMISRI APEWA MECHI YA YANGA vs MAMELOD....'DATA' ZOTE HIZI HAPA...