Home news SIMBA WATWAA UBINGWA MBELE YA COASTAL UNION

SIMBA WATWAA UBINGWA MBELE YA COASTAL UNION


 USHINDI wa mabao 2-0 waliopata Simba leo mbele ya Coastal Union umewatosha kuwafanya watangazwe rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Ni mabao ya John Bocco nahodha wa Simba ambaye alipachika bao dk 13 likiwa ni bao lake la 15 ndani ya ligi na Chris Mugalu dk 23 likiwa ni bao lake la 13.

Unakuwa ni ushindi wa nne mfululizo kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ikiwa imefikisha jumla ya Pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  WASIOOA WAKWAMWA KWA WALIOOA, WANYOOSHWA 3-0, ZACHAPWA KAVUKAVU