Yanga SC

JULAI 15 ITAKUWA NIYONZIMA DAY

admin July 13, 2021 7:47 am


 NYOTA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, Haruna Niyonzima mkataba wake unameguka pale msimu utakapoisha wa 2020/21 kwa kuwa awali aliongeza kandarasi ya miezi sita.

Uongozi wa Yanga umempa mkongwe huyo heshima kwa kumuaga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu FC ambao unatarajiwa kuchezwa Julai 15 Uwanja wa Mkapa.

Taarifa kupitia Ukurasa rasmi wa Instagram ya Yanga imeeleza kuwa Julai 15 itakuwa ni Niyonzima Day na kuwaomba mashabiki waikose siku hiyo.

Kiungo huyo amecheza kwa muda mrefu ndani ya Yanga pia aliwahi kucheza kwa watan zai wa jadi Simba na aliweza kuwa miongoni mwa wachezaji waliotinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa  huko.



VIDEO: NIYONZIMA KUSEPA YANGA, SIMBA KULIPA KISASI KWA YANGA YANGA: TUTAIPIGA SIMBA PALEPALE KWENYE MSHONO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply