Simba SC

NYOTA WA TANO WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC LEO KWA MKAPA

admin July 15, 2021 6:47 am


 WAKATI kikosi cha Simba kikitarajiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex nyota wake watano watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji hao ni pamoja na Jonas Mkude ambaye ni kiungo huyu matatizo yake ni suala la nidhamu.

Ibrahim Ajibu huyu naye ni kiungo naye bado anaumwa Malaria.

Miraji Athuman, aliumia kwenye mazoezi hivyo hataweza kucheza leo mbele ya Azam FC.

Bernard Morrison huyu naye ni kiungo yupo zake nchini Ghana kutokana na matatizo ya kifamilia.

Pia yupo Perfect Chikwende ambaye naye ni kiungo yupo zake nchini Zimbabwe kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Mchezo wa leo Simba haina cha kupoteza kwa kuwa imeshatwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 79 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 64.

Licha ya kutokuwa na cha kupoteza Matola amebainisha kwamba wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa leo.

VIDEO: BASI LA YANGA JIPYA CHOO MPAKA NDANI VIDEO:MORRISON ATIMKA SIMBA, YANGA KUIMALIZA IHEFU KWA MKAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply