BORUSSIA Dortumund wamezima mpango wa Chelsea kuipata saini ya mshambuliaji wao Erling Haaland ambaye alikuwa kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi hicho kwa mujibu wa ripoti kutoka Ujerumani.
Chelsea wanaelewa kwamba uhitaji wao kumpata Haaland ni mkubwa na wamekubali kumtoa Tammy Abraham ama Callum Hudson-Odoi ili iwe sehemu ya mabadilishano ya kukamilisha dili lao.
Haaland,mwenye miaka 20 ambaye anashiriki Bundesliga ametupia jumla ya mabao 20 jambo ambalo limeongeza nguvu kwa Chelsea kuhitaji saini ya nyota huyo ili ajiunge nao ndani ya Ligi Kuu England msimu ujao wakipambana kupata saini ya nyota huyo.
Licha ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea msimu huu imekuwa ikipata tabu kwenye safu ya ushambuliaji hasa mbele jambo ambalo limemfanya Kocha Mkuu, Thomas Tuchel kufikiria kupata saini yake.