Simba SC

GOMES WA SIMBA ASEPA NA TUZO YA KOCHA BORA

admin July 16, 2021 6:47 am


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Juni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, leo Julai 16 imeeleza kuwa Gomes ameshinda tuzo hiyo baada ya kukiongoza kikosi hicho kushinda kwenye michezo mitatu ambayo walicheza.

Michezo hiyo ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting 0-3 Simba, Polisi Tanzania 0-1 Simba na Simba 4-1 Mbeya City.

Pia amewashinda makocha ambao ni pamoja na Nasreddine Nabi wa Yanga pamoja na George Lwandamina wa Azam FC.

Inakuwa ni tuzo ya pili kwa Gomes kwa kuwa ile ya awali alitwaa mwezi Aprili.

NYONI:SIMBA NI TIMU NZURI, MASHABIKI WAJITOKEZE KWA WINGI JUMAPILI JOHN BOCCO ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply