Home Ligi Kuu ACHA LIGI IMALIZIKE SALAMA, ULE UJANJAUJANJA NA MAKANDOMAKANDO YAWEKWE KANDO

ACHA LIGI IMALIZIKE SALAMA, ULE UJANJAUJANJA NA MAKANDOMAKANDO YAWEKWE KANDO


 WAKATI ni ukuta na hakuna ambaye anaweza kuzuia kwa namna yoyote ile hivyo kwa sasa kinachotokea kwenye ulimwengu wa soka sio cha kushangaza bali ni muda hasa kwa zile ambazo zinakwenda kujua hatma yao kama watashuka ama watabaki ndani ya ligi.

Ipo wazi kwamba bingwa wa ligi ni Simba ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa taji hilo kwenye mchezo wake dhidi ya Namungo FC ya Lindi.

Inakuwa ni mara ya pili kwa Simba kukabidhiwa taji hilo mbele ya Namungo FC kwa kuwa msimu uliopita ilipotwaa taji hilo ilikabidhiwa Lindi, Uwanja wa Majaliwa na mchezo ulikamilika kwa sare ya bila kufungana.

Wakati huu presha kwenye nne bora imekamilika kwa kuwa timu zote zimeshajua wapi zitakuwa na hakuna ambacho kitabadilika kwenye nafasi hizo kwa matokeo ya mechi za leo.

Kuanzia nafasi ile ya kwanza mpaka ya nne habari itabaki kuwa hivyohivyo na uhakika wa timu hizo umetokana na matokeo ambayo wameyapata.

Kwa kuwa hakuna haja ya kuwaza tena kuhusu kuwa ndani ya nne bora wimbo mkubwa ni kwa timu zile ambazo zinapambana kushuka daraja pamoja na mpangilio mzima ndani ya 10 bora.

Kwa kuwa ni lalasalama na mechi za mwisho leo basi acha kila kitu kiwe kwenye mpangilio sahihi na wachezaji watimize majukumu yao kwa usahihi bila presha yoyote ile.

Zile ambazo kwa sasa zinapambania nafasi ya kubaki ndani ya ligi zicheze mpira kwa kufuata sheria 17 na ule ujanjauja ambao umekuwa ukiripotiwa kutumika kwa mechi za mwisho.


Kikubwa ni kila mmoja kutambua kwamba kinachotakiwa ni kujituma na kucheza kwa wakati muda huu wa lala salama na makosa ya uwanjani yatumike kuadhibu timu na sio mchezo wan je ya uwanja.

Imekuwa ikiripotiwa kuhusu masuala ya mechi kuuzwa hasa kwa baadhi ya wachezaji na wakati mwingine timu pia kuwa kwenye mpango huo.

Masuala haya hayapaswi kupewa nafasi badala yake mpira uchezwe uwanjani na matokeo yapatikane ndani ya uwanja hakuna kingine.

SOMA NA HII  KMC YAANZA KUIVUTIA KASI YANGA

Ni wazi kwamba msimu huu ulikuwa na mambo mengi mazuri ambapo kila timu ilikuwa na malengo yake mwanzoni na hata mwisho pia malengo yalikuwepo.

Kwa kuwa ilikuwa hivyo basi ni wakati wa kuona kwamba kila timu inamaliza ligi salama na kuanza hesabu za wakati ujao. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 nao upo njiani hivyo maandalizi yanapaswa kuanza kwa sasa.

Waamuzi watimize majukumu yao kwa usawa kwa kuwa kazi yao ni kutimiza sheria 17 za mpira. Yale malalamiko ya mwisho wa mchezo hayapaswi kuwa kwenye mikono yao.

Kinachotakiwa ni kila mmoja kutimiza majukumu yake iwe ni kuanzia kwa wachezaji mpaka mashabiki wao jukumu lao ni ni moja tu kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Ushindani mkubwa unahitajika na nidhamu kwa wachezaji kuwa makini huku kwa upande wa mashabiki nao wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuzipa sapoti timu zao bila kuleta fujo.