kimataifa

CHELSEA KUWATIBULIA MIPANGO UNITED KWA BEKI

admin July 19, 2021 5:47 am


 WAKATI Klabu ya Manchester United ikipiga hesabu ya kuinasa saini ya beki wa Real Madrid, Raphael Varane, Chelsea nayo inatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo kuwatibulia mipango wapinzani wao.

Man United ipo kwenye hesabu za kumpata beki huyo na inaelezwa kuwa ipo kwenye mazungumzo ili kumpata nyota huyo ambaye ametwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa Real Madrid.

Ni dau la pauni milioni 42.8 limewekwa mezani kwa ajili ya kumpata nyota huyo ambaye mkataba wake unakaribia kumeguka msimu huu.

United inaamini kwamba ikakamilisha dili la nyota huyo itaongeza makali hasa kwenye safu ya ulinzi na inatajwa kumpa ofa ya miaka mitano huku Chelsea nayo ikielezwa kuwa wamewasilisha ofa yao ambayo haijawekwa wazi.

GARETH BALE HARUDI TENA TOTTENHAM KAPOMBE: UBORA WA KIKOSI UNATUBEBA, MCHEZO WA YANGA UTAKUWA TOFAUTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply