Home kimataifa PSG YAMPIGIA HESABU POGBA

PSG YAMPIGIA HESABU POGBA


 MAZUNGUMZO kati ya PSG na wawakilishi wa Paul Pogba yanaendelea na makubaliano yapo katika hatua nzuri. Pogba kwa sasa kipaumbele chake ni kujiunga na Paris Saint-Germain.

 

Klabu hiyo bado inatafuta kuimarisha nafasi ya kiungo licha ya kunasa saini ya Wijnaldum kutoka Liverpool. PSG inatazamia wachezaji wawili ambao wamebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika vilabu vyao, mpango A Pogba (28) na mpango B Camavinga (18).

 

Endepo dili la Pogba litashindikana PSG watahamia mpango B ambao ni Camavinga. Na ikumbukwe Manchester United wanamtaka Eduardo Camavinga kama mrithi wa Paul Pogba.

SOMA NA HII  KUMBE RAMOS KUTOITWA TIMU YA TAIFA IMEMUUMA