Uncategorized

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU YANGA

admin July 23, 2021 4:43 pm

 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga, Julai 25.


Simba wakiwa  ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho wanatarajiwa kumenyana na Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika. 



Ni majira ya saa 10:00 jioni mbungi hiyo yenye ushindani mkubwa inatarajiwa kupigwa huku tayari timu zote mbili zikiwa zimeshatia timu mwisho wa reli Kigoma. 


Gomes amesema:”Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu  ambao unahitaji matokeo, katika hilo ninaamini wanalijua.


“Tumekuwa na muda mzuri baada ya kukamilisha lengo la kutwaa taji la ligi sasa kazi imebaki hapa kwenye hili la Shirikisho na hakuna njia ambayo tunaweza fanya zaidi ya kushinda.


“Najua kwamba Yanga nao wapo imara wanahitaji kushinda lakini kwa upande wangu nasema tuliweka wazi kuwa tunahitaji kombe hili tutafanya vizuri, mashabiki watupe sapoti,”.

KOCHA AS VITA AFUNGUKA DILI LA MAYELE KUTUA YANGA GOMES – TUMESHAIMALIZA MECHI DHIDI YA YANGA KITAMBO TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply