Yanga SC

MUKOKO AWAPIGIA MAGOTI UONGOZI WA YANGA

admin July 26, 2021 4:39 pm


KIUNGO wa Yanga, Mukoko Tonombe ameomba radhi  mashabiki, benchi la ufundi pamoja na uongozi wa klabu hiyo kwa ujumla kutokana na kupata  kadi nyekundu dhidi ya Simba.

Mukoko alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko nahodha wa Simba, John Bocco katika fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Mukoko aliandika hivi; “Nachukua fursa hii kuomba radhi mashabiki pamoja na viongozi na benchi la ufundi, kilichotokea katika mchezo wa fainali wa Yanga na Simba;

“Sikukusudiwa kupewa kadi yakupoteza mchezo hu, naipenda sana Yanga, timu yangu, Yanga daima mbele nyuma mwiko,’amesema.

Simba ilipata bao kupitia kwa kiungo mkabaji Thaddeo Lwanga, Yanga ikiwa pungufu, tayari Mukoko alikuwa ameishapewa kadi nyekundu.

 

SIMBA WATAJA SABABU YA KUTOSHIRIKI KAGAME CUP , YANGA WATAJWA KIMEUANA: ZAWADI MAUYA AMSHUKIA MUKOKO KWA KUSABABISHA YANGA IFUNGWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply