kimataifa

ARSENAL YAMPIGIA HESABU LAUTARO

admin July 30, 2021 8:43 am


 IMEELEZWA kuwa Klabu ya Arsenal ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Inter Milan, Lautaro Martinez ili kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

Dau la kumpata nyota huyo ambaye bado ana mkataba ndani ya timu yake linatajwa kuwa ni pauni milioni 77 sawa na shilingi bilioni 246.6 kwa mkwanja wa ardhi ya Tanzania.

Katika orodha ya washambuliaji ambao wanahitajika ndani ya Arsenal yupo pia Tammy Abraham ambaye anakipiga ndani ya Chelsea kwa sasa na thamani yake inatajwa kuwa pauni milioni 40.

Sababu kubwa ya mshambuiaji huyo kuwekwa kwenye hesabu na Arsenal ni uhitaji wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mikel Arteta ambaye anataka kuipata saini ya raia huyo wa Argentina ambaye mkataba wake ndani ya Inter Milan una miaka miwili.

MPANGO WA MANGALO KUMRITHI PASCAL WAWA MSIMBAZI UKO HIVI STRAIKA WA POLISI TZ ALIYEVUNJIKA MIGUU YOTE AMLILIA MAMA SAMIA KWA UCHUNGU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply