Cecafa Cup

YANGA YAMREJESHA JUMA MAHADHI, KUANZA NA KAGAME

admin July 30, 2021 12:44 pm


 STRAIKA wa Yanga, Juma Mahadhi, amerejea kikosini na atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki michuano ya Kombe la Kagame inayoanza keshokutwa Jumapili kwenye viwanja vya Mkapa na Azam Complex jijini Dar es Salaam.


Yanga imemrejesha Mahadhi aliyetolewa kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita huko Ihefu FC Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa Mahadhi alikuwa kwa mkopo Ihefu, hivyo anarejea katika timu yake baada ya muda wa mkopo kumalizika.

 

“Mahadhi amerejea rasmi katika klabu yake aliyokuwa anaichezea akitokea Ihefu tulipompeleka kwa mkopo wa miezi sita pekee.


“Hivyo Mahadhi ataungana na wachezaji wengine watakaokuwepo kwenye kikosi chetu kitakachoshiriki michuano ya Kagame,” alisema Bumbuli

UKIACHANA NA BARBARA, HIZI HAPA SABABU NYINGINE ZA MANARA ‘KUFYEKWA’ MSIMBAZI VIDEO: POLISI TANZANIA WAKANA ISHU YA KUMTELEKEZA MDAMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply