Home Simba SC ADUI NAMBA MOJA WA NYAVU AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

ADUI NAMBA MOJA WA NYAVU AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

 


ADUI namba moja wa nyavu kwa mujibu wa mtangazaji Hasheem Ibwe wa Azam TV , Meddie Kagere amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, kesho ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC.

Katika mchezo huo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imepanga kuwakabidhi taji la ligi ambalo wameshinda kwa msimu wa 2020/21.

Kagere akiwa ametupia mabao 12 ni namba tatu ndani ya Simba ambapo kinara ni nahodha John Bocco mwenye mabao 15.

Nyota huyo amesema:”Mashabiki naomba muje kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia namna ambavyo tutapewa kombe.

“Kwa kuweza kutwaa taji la ligi kwetu ni furaha na tunashukuru kwa sapoti ambayo mmekuwa mkitupa,” .

Msimu uliopita wa 2019/20 Kagere alikuwa namba moja kwa utupiaji ambapo alitupia jumla ya mabao 22.

SOMA NA HII  ACHANA NA BILIONI 20..,HAPA TU NDIPO MO DEWJI ALIPOWASHIKA SIMBA SC