Home Habari za michezo BAADA YA KAZIER CHIEF KUANZA KUJIFIKIRIA KUMCHUKUA NABI….MOSIMANE AINGILIA KATI DILI…ISHU IKO...

BAADA YA KAZIER CHIEF KUANZA KUJIFIKIRIA KUMCHUKUA NABI….MOSIMANE AINGILIA KATI DILI…ISHU IKO HIVI…

Habari za Michezo Bongo

Kocha Mpya wa wa Klabu ya Al Wahda ya Falme za Kiarabu, Pitso Mosimane amempitisha aliyekuwa Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, kufundisha soka Afrika Kusini, huku akihusishwa na mpango wa kuwaniwa na Kaizer Chiefs.

Mosimane amempitisha Nabi, baada ya kufanya mahojiano katika chombo cha habari Afrika Kusini ambako yupo kwa sasa kwa ajili ya Mapumziko mafupi baada ya kuachana na Al Ahli Jeddah, huku akisubiri kuanza majukumu yake mapya katika klabu ya Al Wahda iliyomtambulisha mwishoni mwa juma liilopita.

Akiwa katika Kipindi cha Sport Night Amplified kinachorushwa na Radio Metro FM, Pitso Mosimane alijadili iwapo Nabi atafaa kuifundisha Kaizer Chiefs kwa msimu ujao.

Mosimane alisema: “Ni Mtu poa na ni Kocha Bora” amesema Pisto akimuongelea Nabi.

“Ameshinda trebles Mara mbili, sio Makocha wengi wameweza kushinda Trebles mara mbili. Mimi Nadhani niliipata mara mbili lakini kwa miaka tofauti,lakini yeye aliipata kwa Misimu miwili mfululizo.

“[Lakini] soka la Afrika Kusini si soka la Tanzania. Soka la Tanzania ni Young Africans, Simba SC na Azam na nyinginezo bila kuzidharau timu yoyote”

“Anajua msongo wa mawazo, anajua presha ya kutoa kile watakacho mashabiki. Anajua aina hiyo ya Presha, kwa hiyo nadhani anajua namna ya kupambana na Presha za namna hiyo, na amethibitisha kuwa ni Kocha Bora ndio maana aliifikisha Young Africans fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Natumai anaweza kufanya vyema hata Kaizer Chiefs, ila sina uhakika kwa sababu sijui ubora wa wachezaji wa Kaizer Chiefs, siwezi kuhukumu, kwa sababu siiangalii sana.”

Huku mazungumzo kati ya Nabi na Chiefs yakielezwa kuwa yamekwama kufuatia ombi la kocha huyo wa Tunisia la kutaka kutua klabuni hapo na Benchi lake la Ufundi, Mosimane aliangazia umuhimu wa Kocha kuwa na makocha anaotaka kufanya nao kazi

“Hapana, siwezi,” alielezea alipoulizwa,kama anaweza kujiunga na klabu bila Benchi lake la Ufundi.

“Unafanyaje hivyo? Kwa levo tulizopo lazima uwe na timu yako ya Benchi la Ufundi utayoenda nayo popote.Timu zinapokuajiri, hazikuulizi, zinajua unaenda ukiwa Full Package. Kwa hivyo nina timu yangu ninayoenda nayo Al Wahda.

“Kwenye timu yangu (Benchi langu) tumeongeza mtu,tumemleta kocha wa makipa ambaye nilikuwa naye Al Ahli. Nimemchukua kwa sababu nyingi anazungumza Kiingereza vizuri,anazungumza Kiarabu na pia atanisaidia”

Kauli hiyo ya Mosimane ni dhahir inaunga mkono msimamo wa Nabi dhidi ya Viongozi wa Kaizer Chiefs, ambao wanadaiwa kupinga ombi la Kocha huyo kutua klabuni hapo na timu yake ya Benchi la Ufundi.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa bado mazungumzo baina ya pande hizo yanaendelea na wakati wowote, Nabi na Uongozi wa Kaizer Chiefs watafikia muafaka wa jambo hilo.

Ifahamike kuwa wakati Nabi akiondoka Young Africans kufuatia mkataba wake kufikia kikomo, wasaidizi wake wote katika Benchi la Ufundi katika klabu hiyo nao wamemaliza mikataba yao na kwa sasa wapo huru kujiunga na klabu yoyote itakayowahitaji.

Mpango huo unatazamwa kama mtego kwa Kocha Nabi wa kutaka kuhamia Afrika Kusini na wasaidizi wake ambao alifanyanao kazi kwa mafanikio makubwa akiwa Young Africans, ambayo ameiwezesha kutawala soka la Tanzania Bara kwa msimu miwili mfululizo, huku akitinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kushindwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kanuni ya bao la ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Kocha Minziro anavyowindwa Ligi Kuu 2023/24
Katika mchezo wa mkondo wa Kwanza Hatua ya Fainali Young Africans ilikubali kufungwa 2-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha wakali hao wa Jangwani wakaenda kushinda bao 1-0 ugenini mjini Algers, hivyo timu hizo kimahesabi zilifunga 2-2 kwa matokeo ya jumla.

Bao la ugenini ambalo USM Algers walilipata katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ndilo liliipa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa 2022/23.

SOMA NA HII  KIKOSI BORA CHA LIGI KUU WANAUME NA LIGI KUU WANAWAKE HIKI HAPA