Home Uncategorized NYOTA SABA WAIPASUA KICHWA AZAM FC

NYOTA SABA WAIPASUA KICHWA AZAM FC

YAKUB Mohamed, Daniel Amoah na Razack Abarola wachezaji hawa kwa sasa bado wapo Ghana.

Pia, Bruce Kangwa, Never Tigere na Donald Ngoma hawa wapo Zimbabwe na Nicolas Wadada huyu bado yupo Uganda.


Nyota hawa saba wa kikosi cha kwanza cha Azam FC kilicho chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba bado hawajaripoti kambini kutokana na ‘lockdown’ inayoendelea kwenye nchi zao kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa bado utaratibu wa kuwarejesha unaendelea ili nyota hao wajiunge na kikosi ambacho kimeshaanza mazoezi tangu Mei 27.

SOMA NA HII  CHEKI MOTO WA KIKOSI BORA CHA WIKI CHA SIMBA NA YANGA