Home Yanga SC BAADA YA KUZIDIWA NA SIMBA MSIMU HUU, YANGA WAMKIMBILIA SVEN NCHINI MOROCCO

BAADA YA KUZIDIWA NA SIMBA MSIMU HUU, YANGA WAMKIMBILIA SVEN NCHINI MOROCCO


Uongozi wa Yanga tayari umewapa mapumziko ya wiki mbili wachezaji wake kisha watakusanyika kwenda kambini nchini Morocco mwanzoni mwa wiki ya pili mwezi ujao kujiandaa na msimu ujao.

Morocco ni nchi ya kifalme inayoongozwa na Mfalme Mohamed ambaye miaka ya nyuma alifanya dhiara Tanzania na kukutana na Hayati Magufuli.

Hata hivyo , Yanga wakiwa huko huenda wakakutana na kocha wa zamani wa Simba Sven Vandebroken ambaye anafundisha timu ya AS FAR.

Mshauri wa uongozi wa Yanga, Senzo Mazingiza akizungumza baada ya kurudi jijini Dar es Salaam wakitokea Kigoma alisema wachezaji wamepewa mapumziko wakaonane na familia.

“Wachezaji wanaenda kupumzika wakirudi tuwe na kazi ya kujiandaa na msimu ujao.”

Pia Senzo amesema wamejidhatiti na Yanga ijayo itakuwa imara zaidi na yenye uwezo wa kupambana Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza Septemba 11.

Soka la Bongo inafahamu sehemu kubwa ya kikosi Yanga kitaenda Morocco, lakini wachezaji wengine watabaki Dar kwa ajili ya Kombe la Kagame linaloanza Agosti, mwaka huu.

SOMA NA HII  RAIS WA FIFA NA CAF KUZISHUHUDIA SIMBA NA YANGA KESHO KUTWA....MAJALIWA AWAOA NENO LA KUZINGATIA...