Home Uncategorized YANGA YA GSM YATENGA MILIONI 80 KUMNG’OA ‘HD’ MSIMBAZI..MPANGO MZIMA UKO HIVI..!!

YANGA YA GSM YATENGA MILIONI 80 KUMNG’OA ‘HD’ MSIMBAZI..MPANGO MZIMA UKO HIVI..!!

YANGA wamekutana ijini Dar es Salaam na kukubaliana kuachana na mastaa wa Simba kwenye usajili ujao, lakini siyo Hassan Dilunga ambaye ni kipenzi cha Bilionea wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’.

Yanga wamepanga kuongeza kiungo mshambuliaji mzawa mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi na kufunga na jina la Hassan Dilunga sasa lipo kwa mmoja wa wadhamini wa Yanga, GSM ambao habari zinasema kwamba wameshateta na mchezaji huyo na wamemuwekea Sh80milioni mezani.

Yanga wanaamini kwamba Dilunga ni rahisi kuwa msaada kwamba kwavile aliwahi kuchezea timu hiyo ya Jangwani kuliko kumsainisha Said Ndemla ambaye amekaa Simba miaka mingi na ameshajiwekea mizizi hivyo hata akivuka boda kutakuwa walakini.

Dilunga ambaye anamaliza mkataba wake na Simba mwisho wa msimu, ndiye kiungo mzawa nyota aliyepiga mzigo sana msimu huu akitengeneza nafasi na kutupia mabao.

Tayari GSM wamepewa jina la Dilunga na baada ya kujadiliana Kocha Luc Eymael wameanza mchakato kimyakimya wa kunasa saini ya mchezaji huyo wa zamani wa Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba GSM tayari wameshawasilisha ofa yao mezani kumng’oa mchezaji huyo maarufu kama HD wakitenga kiasi cha Sh80milioni na tayari kiungo huyo amekubali kila kitu.

“Nafikiri atasaini wakati wowote kama ataamua kufanya uamuzi ambao aliahidi mara ya mwisho walipokutana alipopewa ofa na akakubali,” alisema bosi huyo wa Yanga huku Kocha Luc Eymael akisisitiza kwamba; ”Ninasajili kwenye ushambuliaji, kiungo na hata ulinzi lakini ni mapema kutaja majina.”

Meneja wa Dilunga, Zubeir Kambi aliiambia Mwanaspoti jana kwamba mpaka sasa mteja wake ni muajiriwa wa Simba na mkataba unamalizika mwisho mwa msimu hivyo apewe muda hatma itajulikana.

Endapo Yanga itamnasa HD itakuwa ni kama kumrudisha nyumbani kiungo huyo kwani alishawahi kuitumikia kikosi hicho wakati wa enzi za kocha Hans van der Pluijm kabla ya kuondolewa kwa madai kwamba alichuja.

Kama Yanga itamnasa HD huenda safari ikamkuta Mohamed Issa ‘Banka’ ambaye hatahivyo bado viongozi wanazozana kuhusiana na hatma yake ingawa wengi wanataka abakizwe kwani hajatumika ipasavyo.

SOMA NA HII  WAWILI WAONDOKA YANGA