Home news KIKOSI BORA CHA HAJI MANARA KWA MSIMU WA 2020/21, WOTE KUPEWA ZAWADI

KIKOSI BORA CHA HAJI MANARA KWA MSIMU WA 2020/21, WOTE KUPEWA ZAWADI


 KIKOSI bora cha Haji Manara, ambapo wote watapewa zawadi ya viatu na majina yataandikwa. Tuzo itatolewa na Haji mwenyewe katika katika sherehe ambayo ataiandaa yeye mwenyewe:-

Nahodha ni John Bocco atacheza namba 9 anaongoza kwa mabao akiwa na mabao 16.

Mshambuliaji mwingine ni Prince Dube atavaa jezi namba 10 anayovaa Lionel Messi.

Kutoka kushoto ni Luis Miquissone atampa jezi namba 11 atakuwa anacheza upande wa kushoto.

Kutoka kulia ni Clatous Chama atapewa jezi namba 7 atakuwa anatokea kulia.

Kiungo mkabaji ni Taddeo Lwanga na Mukoko Tonombe.


Beki wa kati ni Joash Onyango ambaye atakuwa kati.

Daniel Amoah naye atacheza eneo la ulinzi.

Kushoto atakaa Mohamed Hussein ambaye atavaa jezi namba tatu.

Beki wa upande wa kulia atakuwa ni Shomari Kapombe.

Kipa namba moja atakuwa ni Aishi Manula.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho atakuwa ni Didier Gomes akishirikiana na Francis Baraza ambaye kwa sasa yupo ndani ya Kagera Sugar.

Akiba

Jonathan Nahimana.

Pascal Wawa.

Nicolas Wadada.

Feisal Salum.

Abubakhar Salum.

Tuisila Kisinda.

Chris Mugalu.

SOMA NA HII  SIMBA SC WAIBUKA NA MSIMAMO WAO KUHUSU DILI LA MANZOKI NA LUIS...