Home Simba SC MOHAMED HUSSEIN ACHEKELEA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU BARA

MOHAMED HUSSEIN ACHEKELEA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU BARA


MOHAMED Hussein, nahodha wa Simba amesema kuwa ni furaha kwao kuweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo. 

Juzi, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ilikabidhiwa taji hilo baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Namungo FC.

Kwa msimamo ipo na jumla ya pointi 83 baada ya kucheza jumla ya mechi 34 msimu wa 2020/21.

Hussein amesema:”Kila kitu kipo sawa na ni furaha kwetu kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa ligi na kila mmoja anafurahi kuona tumeshinda.

“Mashabiki wetu wanahitaji shukrani kwa kuwa wamekuwa nasi bega kwa bega hivyo ni furaha kuona tumefanikiwa kufanya hivyo,” .

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA SIMBA IKIPATA USHINDI WA TAABU JANA...'TRY AGAIN' ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA TAMKO JIPYA..