Home Taifa Stars TIMU YA TAIFA U 23 YATINGA FAINALI, KOCHA ASHANGAZWA NA UWEZO

TIMU YA TAIFA U 23 YATINGA FAINALI, KOCHA ASHANGAZWA NA UWEZO


 KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa anashangazwa na uwezo wa wachezaji wake alionao kwa sasa kwa namna ambavyo wanafanya vizuri ndani ya uwanja.

Leo Julai 27, Uwanja wa Bahir Dar, katika mashindano ya CECAFA 2021 yanayofanyika nchini Ethiopia, timu ya taifa ya Tanzania, chini ya miaka 23 imefanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Ni ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudan Kusini ambalo limepachikwa na Kelvin Nashon kwa pigo huru la faulo akiwa nje ya 18 ilikuwa dakika ya 64 na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi.

Kima amesema:”Ninashangazwa na uwezo wa wachezaji wangu hasa ndani ya uwanja, lakini kwangu ninaona ni jambo jema kwani tunahitaji ushindi na ushindani ni mkubwa,” .

Fainali inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo itakuwa ni kati ya Tanzania dhidi ya  Burundi.

Timu hiyo ilipocheza na Uganda ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na ilishinda bao 1-0 ilipocheza na DR Congo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS....NABI AANIKA MUSTAKABALI WAKE NA YANGA...