Home kimataifa POGBA ATASAINI MKATABA NDANI YA MANCHESTER UNITED

POGBA ATASAINI MKATABA NDANI YA MANCHESTER UNITED


 KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema anaamini kuwa kiungo wake Paul Pogba atasaini mktaba mpya na timu hiyo.


Pogba amebakiza mkataba 
wa mwaka mmoja na timu hiyo na amekuwa akielezwa kuwa anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu ujao bure.


Kwa sasa staa huyo anawaniwa na Klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na mwenyewe amekuwa akisema mara kwa mara kuwa anataka kuondoka United.

 

Hata hivyo, baada ya Solskjaer kusaini mkataba mpya na timu hiyo amesema anachotaka kufanya ni kuhakikisha kuwa Pogba atasaini mkataba mpya.


“Mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester United na mwakilishi wa Pogba, kumekuwa na mambo mengi sana kuhusu ishu ya Pogba lakini naamini kuwa kila kitu kitakwenda sawa.


“Kwangu naamini kuwa Pogba atasaini mkataba mpya wa kubaki hapa, hili ni jambo ambalo naliamini sana.

 

“Nimefurahia sana kipindi chote ambacho nimekaa na Pogba hapa United na yeye mwenyewe anafahamu hilo. Hakika naamini kuwa bado anafurahia kuendelea kufanya kazi nami,” alisema kocha huyo.


United tayari wameshakamilisha usajili wa mchezaji mmoja kwenye kipindi hiki cha usajili ambaye ni Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund kwa kitita cha pauni milioni 73.

SOMA NA HII  KUMBE ILE ISHU YA BILIONEA WA CHELSEA KUPEWA SUMU AKIWA UKRAINE IKO HIVI AISEE....