Home Yanga SC YANGA WARUDISHA SHUKRAN KWA MASHABIKI

YANGA WARUDISHA SHUKRAN KWA MASHABIKI

 UONGOZI wa Yanga umewashukuru mashabiki wao ambao walijitokeza kwa wingi jana kuipa sapoti timu hiyo.

Ni katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kigoma mwisho wa reli. 

Licha ya jitihada za wachezaji kusaka ushindi ngoma ilikuwa nzito kwa Yanga kwa kuwa walikubali kuokota bao moja nyavuni. 

Ilikuwa kupitia kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga aliyepachika bao hilo kwa bichwa dakika ya 76 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. 

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Yanga wameandika kwamba shukrani kwa mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu ya Wananchi.

Tayari kikosi kimerejea Dar es Salaam wakiwa na medali za mshindi wa pili na taji limeelekea kwa watani zao Simba ambao nao waharejea Dar.

SOMA NA HII  KISINDA AWA MUHIMILI WA YANGA KWA MIPANGO NDANI YA UWANJA