Home Yanga SC MZEE MPILI: KUNA NGAO YA JAMII, WAKIKAA VIBAYA NAWAPIGA KAMA LIGI

MZEE MPILI: KUNA NGAO YA JAMII, WAKIKAA VIBAYA NAWAPIGA KAMA LIGI

 OMARY Mpili,  maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa bado mechi moja lazima Simba wapigwe kwa kuwa hamna namna.

Mpili awali alibainisha wazi kuwa katika mechi hizo mbili ambazo zimebaki,  wakikaa vibaya watapigwa zote ila bahati mbaya moja Yanga wamepigwa.

Umaarufu wake ulikuwa ghafla  baada ya Julai 3 ubao kusoma Simba 0-1 Yanga ambapo bao la ushindi lilifungwa na Zawad Mauya kwa shuti  lililomshinda Aishi Manula baada ya mpira kumgonga beki Shomari Kapombe.

Kabla ya mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa Mzee Mpili alibainisha kuwa watashinda mbele ya Simba kwa kuwa ana watu na mwisho Yanga ikashinda na kusepa na pointi tatu mazima.

Kuelekea katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Mpili amesema:”Kuna Ngao ya Jamii hiyo nayo wakikaa vibaya nawapiga kama nilivyofanya katika mchezo wa ligi,” .

SOMA NA HII  BAADA YA KUTOLEWA CAF...NGASA KAIBUKA NA JIPYA KUHUSU YANGA...